#Sports

KLABU ZA KPL, NSL YAJIIMARISHA LIGI INAPOREJELEWA

Klabu ya Naivas FC inalenga kuendeleza msururu wa kutopoteza mechi katika ligi ya NSL msimu huu watakapomenyana na Mwatate United Jumamosi hii jijini Nairobi.

Klabu hiyo imeanza kampeni yake kwa kishindo, ikipata ushindi mara 2 na kutoka sare katika mechi 1 mwanzoni mwa msimu, matokeo ambayo yamewaweka katika nafasi ya 3 kwa pointi 7.

Kocha mkuu wa klabu hiyo Elvis Ayani, ameelezea imani katika vijana wake kufanya vyema, akisema kwa sasa kikosi chake kiko imara na hakuna jeraha katika kambi yake.

Kwa upande wao, Mwatate United wamekuwa na mwanzo mbovu, wakiwa katika nafasi ya 16 na pointi 1 katika mechi 3.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KLABU ZA KPL, NSL YAJIIMARISHA LIGI INAPOREJELEWA

AFANDE WAWASILI LIBYA KWA CAF

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *