POLISI WAIMARISHA DORIA NAIROBI
Usalama umeimarishwa katika jiji la Nairobi huku matayarisho ya ibada ya kitaifa ya mazishi ya waziri mkuu wa zamani Raila Odinga yakiendelea.
Polisi wameshika doria katika majengo ya bunge, uwanja wa michezo wa Nyayo na kwenye barabara mbali mbali ikiwemo Bunyala, Lang’ata na Uhuru Highway.
Polisi wameshika doria kuanzia alfajiri, baadhi wakitumia farasi, huku maelfu ya wakenya wakiwa tayari wamewasili katika uwanja wa Nyayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































