TANZANIA YAMULIKWA KWA UKIUKAJI
Serikali ya Tanzania imejipata chini ya darubini ya jamii ya kimataifa kuhusu visa vya ukiukaji wa haki za kibinadamu, shirika la Amnesty International likisema visa hivyo vinaongezeka taifa hilo linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu ambao umewaacha nje viongozi wa upinzani.
Licha ya kusifiwa awali kwa kuondoa vikwazo vya mtangulizi wake John Magufuli, Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan amejipata chini ya shutuma kutoka kwa upinzani na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Visa vya utekaji nyara vimeripotiwa pakubwa, waathiriwa wakiwa viongozi wa upinzani akiwemo kiongozi wa CHADEMA Ali Mohammed mwenye umri wa miaka 69 aliyetoweka na kupatikana ameuawa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































