#Business

KENYA IMEPITISHA SHERIA YA KUTOZA FAINI YA SH20M KWA MAKOSA YA MTANDAONI

Wakenya wataopatikana na hatia ya unyanyasaji wa mtandaoni au makosa mengine ya mtandaoni nchini sasa watakabiliwa na faini ya hadi Sh20 milioni au kifungo cha hadi miaka kumi jela chini ya sheria mpya iliyotiwa saini na Rais William Ruto.

Sheria ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta na Makosa ya Mtandao (Marekebisho) ya mwaka 2024, iliyotiwa saini kuwa sheria Oktoba 15, inaimarisha sheria ya 2018 kwa kuanzisha adhabu kali zaidi kwa makosa kama vile unyanyasaji wa mtandao, wizi wa utambulisho, wizi wa data binafsi na uvunjaji wa data.

Chini ya Kifungu cha 27 kilichorekebishwa, wahalifu wanaopatikana na hatia ya unyanyasaji mtandaoni watatozwa faini isiyozidi Sh20 milioni, kifungo cha hadi miaka kumi jela au vyote kwa pamoja.Mamlaka zinasema masharti hayo mapya yanalenga kupunguza ongezeko la ulaghai mtandaoni, unyanyasaji na maudhui hatari ya kidijitali.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *