MAHAKAMA UGANDA YAAMURU SERIKALI KUWAWASILISHA WANAHARAKATI
Serikali ya Uganda imepewa siku 7 kuweka wazi waliko wanaharakati wa Kenya Bob Njagi na Nicholas Oyoo walioripotiwa kutekwa nyara nchini humo takribani wiki 2 zilizopita na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa usalama.
Kwenye uamuzi wake katika kesi inayohusu haki ya washukiwa kuwasilishwa mahakamani ndani ya saa 24 baada ya kukamatwa, hakimu Peter Kinobe ameiagiza serikali hiyo kuwawasilisha waathiriwa katika hali yoyote ile.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mawakili wa Uganda, huku wenzao wa Kenya wakiongozwa na Martha Karua wakishinikiza kuachiwa kwa wawili hao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































