IPOA YASHUTUMU UVAMIZI DHIDI YA POLISI
Mamlaka ya kutathmini utendakazi wa maafisa wa polisi IPOA imeshtumu ongezeko la visa vya kuvamiwa kwa maafisa wa polisi na raia, kisa cha hivi punde kikiwa cha jana ambapo afisa wa GSU alishambuliwa na kuuawa kwa mshale katika lango la Ikulu ya rais jijini Nairobi.
Afisa mwingine aliuawa nje ya uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta huku mwingine akiuawa katika kituo cha polisi cha Kiganjo, mwenyekiti wa IPOA Isak Hassan akisema visa hivyo vinadhoofisha juhudi za kulinda usalama mbali na kuhatarisha Maisha ya polisi.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, Konstebo Ramadhan Hamisi alidungwa mshale kwenye mbavu na mshukiwa kwa jina Kithuka Kinyumi mwenye umri wa miaka 56 katika Gate D ambako umma hutumia kuingia Ikulu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































