FKF YATANGAZA UAJIRI KWA JUNIOR STARS
Shirikisho la soka nchini FKF limetangaza kuwa wazi nyadhifa mbali katika benchi ya kiufundi ya timu ya taifa ya wanaume ya soka kwa wachezaji walio chini ya miaka 17 Junior Stars na kuagiza uteuzi mpya mara moja.
Junior Stars wanajiandaa kwa mechi za kufuzu kwa mashindano ya ubingwa wa bara Afrika yaani 2026 AFCON U-17.
Kupitia taarifa, katibu mkuu wa FKF Harold Ndege, amesema kuwa wameamua kutangaza wazi nafasi hizo kufuatia ukaguzi wa idara ya maendeleo ya soka FDD.
Miongoni mwa nafasi zilizo wazi ni Pamoja na kocha mkuu, msaidizi wa kocha mkuu, kocha wa makipa, msimamizi wa kikosi, na daktari.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































