WAKENYA WAMIMINIKA JKIA
Huzuni imetanda katika uwanja waw a ndege wa kimataifa JKIA ambako maelfu ya wakenya wamewasili kusubiri mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
Wengi wa waliowasili wameonekana wakitokwa na machozi, baadhi wakiwa wamevalia nguo zenye picha ya kinara huyo wa ODM.
Matayarisho yanaendelea katika maeneo mbali mbali ambako mwili wa Odinga utapelekwa hii leo yakiwemo majengo ya bunge, bunge likijiandaa kutoa heshima za mwisho hii leo kuanzia saa nne asubuhi hadi usiku wa manane.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































