THE GAMBIA WATEUA KIKOSI
Timu ya taifa ya wanawake ya Gambia imetaja kikosi cha wachezaji 23 watakaomenyana na Harambee Starlets Ijumaa wiki hii jijini Nairobi katika mkondo wa kwanza wa awamu ya mwisho ya kufuzu fainali za ubingwa wa bara Afrika kwa wanawake WAFCON.
Starlets watakuwa wenyeji wa mkondo wa kwanza ugani Nyayo, kabla ya marudiano siku 4 baadaye ugani Stade Lat Dior nchini Senegal kutokana na Gambia kukosa uwanja uliofikiwa viwango vya CAF.
Kikosi cha Gambia kinachonolewa na Mariama Sowe, kinawajumuisha wachezaji 5 wanaosakata soka ya kulipwa ughaibuni.
Miongoni mwao ni viungo Mariama Cham, Manyima Stevelmans, Fatoumata Cham, Ola Buwaro na mshambulizi Mam Drammeh.
The Gambia ambao wanaorodheshwa katika nafasi ya 124 katika jedwali la FIFA, inasaka kushiriki mashindano ya WAFCON kwa mara kwanza.
Kwa upande wao, Starlets wanaorodheshwa katika nafasi ya 140, na wanasaka tiketi ya mara ya pili baada yao kushiriki mwaka wa 2016.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































