#Local News

BUNGE KUMWOMBOLEZA ODINGA ALHAMISI

Bunge limetenga vikao vya leo kumwomboleza waziri mkuu wa zamani Raila Odinga aliyefariki mapema jana kutokana na matatizo ya moyo alipokuwa akifanya matembezi ya asubuhi nchini India alikokuwa akitibiwa.

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, amesema vikao hivyo vitaanza saa nne asubuhi hadi usiku, ili kuwapa wabunge fursa ya kumkumbuka Odinga kwa mchango wake katika siasa za Kenya alipokuwa mbunge, Waziri mkuu na kiongozi wa upinzani.

Maombolezo bungeni yalianza jana kwenye kikao kifupi, ambako kiongozi wa walio wengi Kimani Ichung’wa na mwenzake wa wachache Junet Mohammed alipewa fursa ya kuomboleza kabla ya kujiunga na ujumbe uliokwenda India.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

BUNGE KUMWOMBOLEZA ODINGA ALHAMISI

SERIKALI YATANGAZA IJUMAA KUWA HOLIDEI

BUNGE KUMWOMBOLEZA ODINGA ALHAMISI

ODINGA KUREJESHWA NCHINI LEO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *