NYOKABI MIONGONI MWA WANAOLENGA KUWA MAJAJI
Tume ya huduma za mahakama JSC imewaorodhesha watu 100 atakaohojiwa kujaza nafasi za majaji 20 wa mahakama kuu, akiwemo aliyekuwa mwakilishi wa kike kaunti ya Nyeri Priscilla Nyokabi.
Kupitia notisi, JSC imesema ilipokea maombi 377 kufuatia angazo ililochapisha kabla ya kuwateua 100 hao.
Miongoni mwa walioorodheshwa na majaji wa mahakama za chini wanaolenga kupandishwa ngazi, Pamoja na mawakili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































