#Local News

WAUGUZI ISIOLO WASITISHA MGOMO

Wakazi wa kaunti ya Isiolo wamepata afueni baada ya wauguzi kutia Saini mkataba wa kurejea kazini na hivyo kutamatisha mgomo wao uliokuwa umesambarataisha huduma za matibabu kwa miezi 2.

Mgomo huo umesitishwa kufuatia mazungumzo kati ya muungano wa wauguzi, bodi ya uajiri wa umma na saerikali ya kaunti hiyo, wauguzi wakitakiwa kurejea kazini kufikia Alhamisi wiki hii.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *