RUTO AWEKA WAZI AFYA YA ODINGA KABLA YA KIFO
Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga alianza kuwa na changamoto za kiafya takribani miezi 2 iliyopita kabla ya kuafikiana na familia kwamba asafarishwe nchini India kwa matibabu.
Haya ni kwa mujibu Rais William Ruto aliyezungumza hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu hali ya afya ya Odinga wakati wa hafla ya mazishi ya kinara huyo wa zamani wa upinzani.
Kulingana na Rais, uamuzi wa Odinga kuelekea India uliafikiwa walipokutana nyumbani kwa Odinga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































