#Sports

EPL KUREJEA ARSENAL WAKIPATA PIGO

Ligi ya soka nchini Uingereza inaingia mechi ya 8 wikendi hii huku klabu ya Arsenal ikikadiria majeraha kwa wachezaji wake muhimu.

Miongoni mwa wachezaji wanaohifwa kukosa mechi ya Arsenal na Fulham ni Martin Zubimendi na Ben White kutokana na majeraha.

Kwenye mazoezi hapo jana, Zubimendi hakuhudhuria huku White akilemewa na kuonekana akipokea matibabu pembeni pa uwanja wa mazoezi.

Wawili hao wanajiunga na Noni Madueke na Kai Havertz kwenye mkeka wa majeraha, ingawa kocha mkuu Mikel Arteta amesema Madueke na Havertz wanaendelea vizuri na huenda wakarejea mapema mwezi ujao.

Hata hivyo, The Gunners watajivunia kurejea mazoezi kwa mara ya kwanza kwa beki Piero Hincapie tangu alipopona jeraha la nyonga.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

EPL KUREJEA ARSENAL WAKIPATA PIGO

RUTO, UHURU WAKUTANA NYAYO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *