ODM YAPATA PAA MAGARINI
Chama cha ODM kimepigwa jeki katika uchaguzi mdogo wa Magarini kaunti ya Kilifi baada ya mwaniaji wa kiti hicho kupitia chama cha PAA Michael Kingi kujiondoa ili kumuunga mkono mwaniaji wa ODM Harrison Kombe.
Kupitia taarifa, PAA imesema kujiondoa kwa Kingi kumetokana na mashauriano na viongozi wengine waliojumuishwa kwenye serikali jumuishi.
Aidha, PAA imesema uamuzi huo unaishia kwenye uchaguzi mdogo ila kitamuunga mkono Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































