SERIKALI KUUNDA HAZINA YA MIUNDOMBINU YA KSH4 TRILIONI KWA MIRADI MBALI MBALI
Rais William Ruto ametangaza mipango ya kuunda Hazina ya Kitaifa ya Miundombinu ya Ksh4 trilioni ili kufadhili miradi mikubwa ya nishati, barabara na mabwawa.
Akiongea wakati wa kuanzishwa kwa Awamu ya Kwanza ya Konza Technopolis katika Kaunti ya Makueni, Ruto amesema hazina hiyo itakusanya rasilimali kutoka kwa bajeti, sekta ya kibinafsi, na ubinafsishaji ili kuendeleza ukuaji wa viwanda nchini.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, rais amefichua kuwa shilingi trilioni 1 itapanua uwezo wa umeme kwa megawatt 10,000, shikingi trilioni 1.5 itajenga mabwawa 50 kwa ajili ya umwagiliaji, na shilingi trilioni 1.5 nyingine itatengeneza barabara kuu mpya, kupanua SGR, na kuifanya JKIA kuwa ya kisasa.
Akitoa mfano wa maendeleo ya Korea Kusini, Ruto alibainisha kuwa uwekezaji wa ujasiri utaongeza ukuaji, na kuongeza kuwa jiji lenye hadhi ya juu la Konza, ndilo litakaloendesha mabadiliko ya kiteknolojia na kiuchumi nchini Kenya.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Ahadi ya Rais William Ruto ya kubuni nafasi za kazi milioni 1.2 kila mwaka bado haijatimizwa, kwani ripoti ya Ofisi ya Bunge ya Bajeti (PBO) inaonyesha ni ajira rasmi 78,600 pekee ziliundwa mwaka wa 2024, ikilinganishwa na kazi 782,300 zisizo rasmi.
Ripoti hiyo pia inaonyesha ukuaji wa uchumi wa Kenya ulipungua hadi 4.7% mnamo 2024 kutoka 5.7% mnamo 2023, kiwango cha chini zaidi tangu janga hilo. Kupungua huko kulichangiwa na utendaji hafifu katika kilimo, ambao ulishuka hadi 3.9%, na kupungua kwa viwanda hadi 1.5%, kutokana na kupungua kwa pato la saruji, viwango vya juu vya riba, na upatikanaji mdogo wa mikopo.
Sekta ya huduma pia ilishuka hadi 6.1% kutokana na shughuli za polepole katika usafiri, fedha, na ukarimu. Wakati mfumuko wa bei ukisalia ndani ya lengo, PBO ilionya kuwa bei za vyakula zinaweza kupanda kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































