KAMPENI YA CAF KUKAMILIKA KESHO
Kampeni ya mataifa ya bara Afrika kuwania tiketi ya kufuzu kwa kipute cha Kombe la dunia mwaka ujao kitakamilika hapo kesho, wakati jumla ya mechi 17 zimesalia kabla ya kutamatika kwa kameni hiyo.
Jumla ya mechi 8 zitachezwa hii leo katika makundi mbali mbali.
Tayari timu za Algeria, Ghana, Morocco, Misri na Tunisia zimefunzu moja kwa moja baada ya kuongoza makundi yao, Ghana ikiwa ya hivi punde kupata tiketi hiyo baada ya mchezaji wa Tottenham Mohammed Kudus kufunga bao la pekee la mchezo dhidi ya Central Africa Republic hapo jana.
Indomitable Lions wa Cameroon watahitaji ushindi kwenye mechi yao ya leo dhidi ya Angola huku wakiomba Cape Verde ipoteze dhidi ya Eswatini ili kujikatia tiketi ya moja kwa moja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































