#Sports

HAALAND AWAKA MOTO EPL

Mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland ameendelea kuonyesha ustadhi wake mbele ya lango baada ya kufunga bao lake la 9 katika ligi kuu nchini Uingereza EPL hapo jana.

Bao la pekee la raia huyo wa Norway liliipa City ushindi muhimu dhidi ya Brentford, City wakichupa hadi nafasi ya tano, alama 3 nyuma ya vigogo Arsenal katika msimamo mpya wa jedwali.

Haaland ambaye ameifungia City mabao 12 msimu huu na mabao 6 kwa timu yake ya kitaifa ya Norway, amesema fomu yake nzuri ya ufungaji wa magoli inatokana na muda wa kucheza na mwanawe wa kiume mchanga aliyezaliwa maajuzi.

Haaland mwenye umri wa miaka 25 ameifungia City mabao 94 katika mechi 104 tangu kuwasili kwake kutoka Borussia Dortmund mwaka wa 2022.

Kwa sasa anamezewa mate na Rais wa Barcelona Joan Laporta, anayeripotiwa kupanga kuweka ofa yake kwa mshambulizi huyo.

Katika msimamo wa ligi, Arsenal wako kileleni kwa alama 16, alama 1 mbele ya bingwa mtetezi Liverpool waliopoteza mechi yao ya pili mfululizo la ligi, nay a 3 kwa jumla baada ya kupokezwa kichapo cha mabao 2:1 na Chelsea.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HAALAND AWAKA MOTO EPL

MOMBASA UNITED WAONYESHA MAKALI NSL

HAALAND AWAKA MOTO EPL

UBASHIRI WAONYA KUHUSU MAFURIKO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *