#Sports

MAN UNITED YAZIDISHA MASAIBU YA LIVERPOOL

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza EPL Liverpool wamepoteza mechi 4 mfululizo, ikiwa na mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 11 baada ya kupokezwa kipigo cha mabao 2:1 nyumbani na Manchester United.

United wanaonolewa na Ruben Amorim waliweka kando masaibu yao na kuanguka na miamba hao wa Uingereza, wakishinda mechi 2 za ligi mfululizo kwa mara kwanza tangu kuwasili kwa Amorim mwaka jana.

Bryan Mbeumo aliiweka United kifua mbele baada ya sekunde 61 za mchezo, kabla ya bao lake kufutwa na Cody Gakpo wa Liverpool katika dakika ya 78.

Hata hivyo, beki wa United Harry Maguire aliwarejeshea uongozi dakika ya 84.

Kichapo hicho kinawashusha Liverpool hadi nafasi ya 4, alama 4 nyuma ya vigogo Arsenal walio na alama 19 baada ya ushindi wa bao 1:0 dhidi ya Fulham.

Katika matokeo mengine, mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland alifunga mabao 2 na kuwapa Ciy ushindi wa mabao 2:0 nyumbani dhidi ya Everton, City sasa wakiwa katika nafasi ya 2 kwa alama 16.

Mabao hayao yanamaanisha kwamba Haaland amefunga mabao 23 katika mechi 13 za taifa lake la Norway na klabu ya City msimu huu, huku akiongoza chati za EPL kwa mabao 13.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAN UNITED YAZIDISHA MASAIBU YA LIVERPOOL

 KIKOSI CHA TAEKWONDO KENYA CHATAJWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *