#Local News

MATIANG’I AZUNGUMZIA MAUAJI YA MTO YALA

Waziri wa zamani wa usalama Dakta Fred Matiang’i, amevunja kimya chake kuhusu mauaji yaliyogonga vichwa vya habri alipokuwa waziri, ikiwemo miili kupatikana katika mto Yala na mauaji ya aliyekuwa afisa wa IEBC Chris Musando.

Kwenye mahojiano yaliyopeperushwa na runinga moja hapo jana, Matiang’i amesema kuwa yuko tayari kufika mahakamani iwapo ataagizwa kufanya hivyo, akiilaumu serikali ya sasa kwa kushindwa kuendesha uchunguzi.

Matiang’i amekariri kuwa aliondoka afisini uchunguzi ukiwa unaendelea, huku akiilaumu idara ya NIS kutokana na madhara ya maandamano ya hivi maajuzi.

Imetayarishwa na Tonny Nyongesa

MATIANG’I AZUNGUMZIA MAUAJI YA MTO YALA

UPINZANI WAMTAKA MURKOMEN NJE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *