315 WAMEANGAMIA KWENYE MAFURIKO, SERIKALI YASEMA

Watu 315 wameaga dunia kutokana na mafuriko hapa nchini, 38 hawajulikani waliko huku 293,205 wakiachwa bila makao baada ya makazi yao kusombwa na maji ya mafuriko. Akiwahutubia waandishi wa habari katika jumba la Nyayo jijini Naiorbi, msemaji wa seriklai Isaac Mwaura, amesema wakenya takribani 306,522 wameathirika na mafuriko hayo, akitangaza kwamba kuna uwezekano mvua hiyo […]

RUTO AZINDUA BWAWA LA KABKARA BUNGOMA

Rais William Ruto amezindua rasmi bwawa la maji la Kabkara katika eneo bunge la Sirisia kaunti ya Bungoma kwa lengo la kutatua uhaba wa maji ambao umekuwa ukishuhudiwa eneo hilo. Akizungumza katika hafla hiyo, amesema mradi huo utawafaidi wenyeji katika masuala ya kilimo, na kuahidi shilingi milioni 300 kwa ajili ya kuimarisha miundomsingi ya bwawa […]

MWAURA: SERIKALI INAIMARISHA KILIMO MAGHARIBI

Huku taifa likijiandaa kwa maadhimisho ya sherehe za 61 za Madaraka hapo kesho ambayo kauli mbiu yake ni kilimo na utoshelezi wa chakula, serikali imetambua eneo la Magharibi mwa nchi kama lenye uwezo wa ukulima, kutokana na mazao mbali mbali yanayozalishwa nae neo hilo. Akiwahutubia wanahabari katika jumba la Nyayo jijini Nairobi, msemaji wa serikali […]

AU YAFUNGUA MILANGO KWA WAGOMBEA WA MWENYEKITI WA AU

Muungano wa Afrika AU umefungua milango yake kwa wagombeaji zaidi katika uchaguzi ujao wa mwenyekiti wa tume ya AU kuwasilisha nakala zao au kujiondoa. Tarehe hizo mpya zina maana kwamba wapinzani sharti wawasilishe kwa mataifa yao stakabadhi zao za wasifu ,taarifa ya maono na jinsi wanavyonuia kuangazia maswala ibuka barani afrika. Hatua hii ni ya […]

KESI YA MAUAJI YA SHARON OTIENO INAENDELEA KUSIKILIZWA

Mpelelezi mkuu wa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno anatarajiwa kuhojiwa leo hii na upande wa utetezi katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa gavana wa Migori Okoth Obado. Mnamo mei kumi mpelelezi aliiambia mahakama kwamba msaidizi wa Obado Michael Oyamo alipanga matukio yaliyosababisha mauaji ya Sharon. Nicholas Olesena amesema kwamba […]

MAHAKAMA YA UPEO YAFUTILIA USHINDI WA HARRISON GARAMA KOMBE

Mahakama ya upeo imedumisha uamuzi wa mahakama kuu na mahakama ya rufaa wa kufutilia mbali ushindi wa mbunge wa magarnini Harrison Garama Kombe Kombe alichaguliwa kupitia tiketi ya chama cha ODM alimshinda mpinzani wake wa karibu kwa kura 21 pekee. Jopo la majaji watano wa mahakama limeamua kwamba mlalamishi Stanley Kinga Karisa alidhibitisha madai yake […]

AKAUNTI YA UDA YA FACEBOOK YADUKULIWA, MALALA

Katibu  Mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala ameibua madai kwamba ukurasa wa Facebook wa Chama hicho umedukuliwa na watu wasiokuwa wanachama wa baraza la uongozi na kwamba tayari amewasiliana na makao makuu ya mtandao huo ili kurekebisha hali Hata hivyo mtaalamu wa mtandao wa rais William Ruto Dennis Itumbi amepuuza kauli ya Malala akisema […]

MILIPUKO YA MAGONJWA KUATHIRI SEKTA ZA BIASHARA BARANI AFRIKA

Ripoti kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki (IGAD) inaonyesha kuwa pembe za Afrika imerekodi ongezeko la milipuko ya magonjwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha mafuriko makubwa. Hata hivyo, IGAD imezitaka nchi ambazo zinashuhudia milipuko hiyo kuweka mikakati kabambe ya misaada na njia za kupata fedha ili kulinda Maisha ya […]

SERIKALI IMEZINDUA MPANGO WA KUBORESHA BIASHARA YA NJE YA NCHI

Serikali kuu imezindua mpango unaolenga kupiga jeki biashara ya nje ya nchi kwa asilimia 10 kwa mwaka kutoka shilingi trilioni moja zilizorekodiwa mwaka jana. Mwenyekiti wa Mamlaka ya Biashara za Nje Jaswinder Bedi amesema kuwa mpango huo unatumika kama ramani ya kulifanya taifa la Kenya kuwa nchi ya uchumi unaoongozwa na biashara ya nje na […]

RUTO AWASHAURI MAAFISA WA JESHI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA UADILIFU

Rais William Ruto amewashauri maafisa ambao wamefusu kutoka taasisi ya kijeshi kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu. Akihutubu katika hafla ya kufuzu kwa maafisa hao rais aidha amewashauri kuwaheshimu wadogo wao kazini ili kukuza ushirikiano bora wakitekeleza majukumu yao. Imetayarishwa na Janice Marete