MAHAKAMA YAZUIA NYONGEZA YA ADA ZA ARDHI KAHAWA
Wakazi wa Kahawa Sukari kaunti ya Kiambu wamepata afueni ya muda baada ya mahakama kuu kutoa amri ya kuzuia serikali ya Kiambu dhidi ya kutekeleza nyongeza ya ada za ardhi hadi kesi itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Kwenye uamuzi wake, jaji Mogeni ameagiza kuwa amri ya muda itolewe ili kuzuia utekelezaji huo hadi mwafaka utakapotolewa.
Kulingana na wakazi waliowasilisha kesi mahakmanai, walikuwa wakilipa shilingi 1,500 kwa mwaka ila serikali hiyo ikapandisha hadi shilingi 15,750 mwaka wa 2024
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































