#Football #Sports

DROO YA ROBO FAINALI YA FA CUP KUANDALIWA

Jumla ya timu 8 zinasubiri kufahamu wapinzani wao katika awamu ya robo fainali ya dimba la FA Cup nchini Uingereza baada ya kufuzu katika mechi zilizosakatwa Jumamosi na hapo jana.

Manchester City walifuzu awamu hiyo baada ya kutoka chini na kuandikisha ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle United ugani St. James Park.

Ushindi wao ulijiri baada ya Arsenal awali kupata ushindi mwembamba wa mabao 2-1 dhidi ya Mansfield, huku Chelsea wakilazimika kuingia muda wa ziada kabla ya kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Wrexham.

Katika matokeo yaliyowaacha wengi vinywa wazi, Southampton inayoshiriki ligi ya Championship iliwabandua Fulham wa ligi kuu, baada ya kuwapa kichapo cha bao 1-0.

Bao la pekee la mchezo lilifungwa na Ross Stewart katika dakika za majeruhi kupitia mkwaju wa penalti.

Timu nyingine zilizofuzu ni Liverpool baada ya kuandikisha ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Wolves, Leeds United na Portvale waliowabandua Sunderland.

Mechi ya mwisho ya kufuzu robo fainali itachezwa hii leo kati ya Brentford na West Ham, ambao matumaini yao pekee yamewekwa kwenye dimba hilo baada ya kukodolewa macho na uwezekano wa kushushwa daraja.

Mechi hiyo itachezwa baada ya droo kufanyika.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *