POLICE FC, GOR WASAKA POINTI KPL
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka, KPL, Police FC, watalenga kuimarisha kampeni yao ya kutetea taji hilo watakapoialika Mara Sugar ugani Police Sacco hii leo.
Kocha mkuu wa Maafande hao Dusan Stojanovic amekairiri kuwa kikosi chake kiko tayari kusistisha msururu wa matokeo duni uwanjani, akisema lengo lao ni kushinda kila mechi.
Police walio katika nafasi ya 7 wakiwa na pointi 23, hawana budi ila kushinda mechi ya leo iwapo wanalenga kutwaa ubingwa wa pili.
Naye kocha mkuu wa Mara Sugar Edward Manoah, amesema licha ya Police kuwa hatari wakiwa nyumbani, vijana wake hawaogopi pingu.
Pambano jingine ni Gor Mahia dhidi ya Murang’a Seal, Gor wakilenga kuvuna ushindi baada ya sare ya kutofungana dhidi ya Shabana Jumapili iliyopita na kuwapa nafasi washindani wao AFC Leopards nafasi ya kufungua mwanya wa pointi 3 mbele yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































