TUKO SERIKALINI, ODM
Chama cha ODM kitaendeleza ushirikiano wake na serikali ya Kenya Kwanza hadi mwaka 2027 na kwamba hakuna mgawanyiko chamani kuhusu ushirikiano huo.
Haya yamebainika kwenye mkutano wa kwanza wa kamati kuu ya chama hicho tangu kifo cha aliyekuwa kinara wake Raila Odinga.
Kwenye taarifa iliyosomwa na katibu mkuu Edwin Sifuna, ODM imetangaza kufanya mkutano maalum wa kuadhimisha miaka 20 ya chama hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































