#Football #Sports

NAIROBI UNITED WAANDIKISHA TAARIFA

Klabu ya soka ya Nairobi United inayoshiriki ligi kuu ya soka KPL imeandikisha ukurasa mpya katika historia ya soka nchini baada ya kuwa klabu ya kwanza kuingia awamu ya makundi katika mashindano ya ubingwa wa mashirikisho ya mabara ya CAF yaani CAF Confederations Cup katika jaribio la kwanza.

Naibois, jinsi wanavyofahamika kwa jina la utani, wamefuzu awamu baada ya kupata ushindi wa mabao 7-6 dhidi ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia kupitia mikwaju ya penalti.

Hii ni licha ya kichapo cha mabao 2-0 hapo jana kwenye mkondo wa pili, na hivyo kufanya mambo kuwa jumla ya magoli 2:2 kufuatia ushindi wao sawa katika mkondo wa kwanza.

Vijana hao wa Nairobi United walipata tiketi ya kufuzu mashindano ya CAF Confederations Cup baada ya kutawazwa mabingwa wa Kenya Cup mwishoni mwa msimu jana, msimu ambao pia walipandishwa daraja kushiriki KPL.

Kufuzu kwao ni hatua kubwa kwa klabu ambayo ni maajuzi tu imepandishwa daraja, mbali na kupata mataji mawili katika msimu huo.

Kwa sasa ndio wawakilishi wa pekee wa Kenya katika jukwaa la bara Afrika, baada ya Police FC kubanduliwa na Al-Hilal ya Sudan katika awamu sawa ya mashindano ya klabu bingwa barani Afrika.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

NAIROBI UNITED WAANDIKISHA TAARIFA

HARAMBEE STARLETS WAIMARISHA MAANDALIZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *