MATOKEO YA KJSEA KUTOLEWA
Watahiniwa zaidi ya milioni 1.1 waliofanya mtihani wa kitaifa wa gredi ya 9 KJSEA watafahamu matokeo ya mtihani huo hii leo, ukiwa ni mtihani wa kwanza kabisa tangu kufutiliwa mbali kwa KCPE.
Tofauti na KCPE ilioibua ubabe wa shule, matokeo ya KJSEA yatamlenga mtahiniwa binafsi na wala si uorodheshaji wa shule au mashindano kati ya watahiniwa.
Watahiniwa watapokea matokeo yao kupitia tovuti ya baraza la mitihani ya kitaifa KNEC baada ya kuwekwa wazi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































