AFUENI YA SARATANI
Wagonjwa wanaosaka matibabu ya saratani nchini wamepata afueni kufuatia hatua ya serikali kuongeza fedha inazolipia matibabu yao kutoka shilingi elfu 550 hadi elfu 800 kwa mwaka chini ya mpango wa afya ya jamii SHA.
Kwenye hotuba yake kwa taifa kupitia bungeni, Rais William Ruto amesema malipo hayo yataanza kutolewa mwezi ujao, huku akitetea bima ya SHA anayosema imewasaidia wananchi wengi wa kawaida kupata huduma za matibabu.
Aidha, amepigia debe mpango wa afya ya wote, akisema umefaidi wakenya hasa maeneo ya mashinani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































