WAKENYA URUSI: OMTATAH KUISHTAKI SERIKALI
Seneta wa Busia Okiya Omtatah, ametangaza mpango wa kuwasilisha kesi mahakamani kuishtaki serikali kutokana na kinachoonekana kama kushindwa kuzuia mtandao wa ulaghai unaowasafirisha wakenya kupigana katika vita baina ya Ukraine na Urusi.
Tangazo hilo linajiri huku familia kadhaa nchini zikiachwa na majonzi baada ya kushindwa kuwarejesha nchini jamaa zao waliofariki wakipigana kwenye vita hivyo.
Omtatah ameitaka serikali kufafanua mpango wa Ajira Majuu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































