UPINZANI WAMLIKA IEBC MBEERE NORTH
Muungano wa upinzani umeibua madai kwamba tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC inawasajili wapiga kura wapya katika eneo bunge la Mbeere North kinyume na sheria, ikizingatiwa kuwa eneo hilo linajiandaa kwa uchaguzi mdogo.
Kulingana na upinzani ukiongozwa na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, hatua hiyo ya IEBC inalenga kuiba kura kwenye uchaguzi huo mdogo utakaondaliwa chini ya wiki 2 zijazo.
Hata hivyo, upinzani umeonyesha matumaini ya mgombeaji wao Newton Karish kuibuka na ushindi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































