#Football #Sports

BARCELONA YAREJEA KILELENI MWA LA LIGA

Klabu ya FC Barcelona ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Levante  na kurejea kileleni mwa msimamo wa La Liga .

Baada ya Real Madrid kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya  Osasuna , kikosi cha kocha Hansi Flick kilipanda kileleni kwa tofauti ya alama moja kufuatia ushindi huo uliopatikana katika uwanja wa Camp Nou.

Marc Bernal na Frenkie de Jong waliipa Barcelona uongozi wa mapema katika kipindi cha kwanza, huku Fermin Lopez akihitimisha ushindi huo kwa shuti kali katika dakika za mwisho.

Barcelona walihitaji ushindi huo kurejesha morali baada ya kuchapwa mabao 4-0 na Atletico Madrid katika nusu fainali ya kwanza ya Copa Del Rey, na baadaye kupoteza 2-1 dhidi ya Girona FC kwenye ligi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

BARCELONA YAREJEA KILELENI MWA LA LIGA

MAN UNITED KUTAFUTA USHINDI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *