IEBC YATAKA BILIONI 1 KWA MAAKULI
Wabunge wametofautiana na bajeti ya shilingi bilioni 63.9 ya tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, ambapo shilingi bilioni 1 zimetengewa chakula cha maafisa wa tume hiyo katika kipindi cha uchaguzi.
Wakifika mbele ya kamati ya haki na masula ya kisheria bungeni, maafisa wa IEBC wamesema kwamba wanahitaji shilingi bilioni 1 kufanikisha kutuma matokeo ya uchaguzi, bilioni 5.9 za kuchapisha karatasi za uchaguzi, na bilioni 6.2 za kubadilisha vifaa vya KIEMS.
Hata hivyo, wabunge wamekosoa bajeti hiyo, wakisema ni ghali zaidi kwa uchaguzi mkuu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































