#Business

KANUNI MPYA ZA KRA ZA KUKUSANYA USHURU MWAKA HUU

Mamlaka ya kukusanya Ushuru nchini (KRA) imebadilisha jinsi inavyokagua ripoti za ushuru wa mapato, na hivyo kuashiria mabadiliko makubwa katika utekelezaji wa ushuru. Tangia mwezi Januari mwaka huu, mamlaka hiyo itathibitisha kila takwimu iliyotangazwa katika marejesho ya kodi ya mapato dhidi ya data ya kielektroniki ya wakati halisi wakati wa kuwasilisha.

Chini ya mfumo mpya, rekodi za KRA zimetangaza mapato na gharama kwa kutumia data kutoka Mfumo wa Kielektroniki wa Kusimamia mfumo wa Ushuru (eTIMS), rekodi za zuio la ushuru, na maelezo ya uagizaji wa forodha.

Hapo awali, walipa kodi waliwasilisha marejesho ya ripoti ya mapato ya kila mwaka, ambayo KRA ilikagua baadaye kupitia ukaguzi au maswali. Mchakato huo pia uliruhusu nafasi ya maelezo baada ya kuwasilisha. Hata hivyo, Mbinu hiyo mpya ina uwezo wa kuwezesha utekelezaji wa kiwango cha juu zaidi, huku uthibitisho ukifanyika papo hapo marejesho yanapowasilishwa.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

KANUNI MPYA ZA KRA ZA KUKUSANYA USHURU MWAKA HUU

ARSENAL WATINGA FAINALI TANGU 2018

KANUNI MPYA ZA KRA ZA KUKUSANYA USHURU MWAKA HUU

KINDIKI: NYOTA KUWAFIKIA MILIONI 2

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *