#Basketball #Sports

KENYA YAVUNJA REKODI BARANI AFRIKA MPIRA WA VIKAPU

Kenya imevunja rekodi ya kuwa timu ya kwanza barani Afrika kufuzu katika kategoria mbili za wanawake na wanaume katika mashindano ya Commonwealth ya mchezo wa vikapu wa 3×3 yatakayoandaliwa jijini Glasgow, Scotland baadaye mwaka huu.

Timu ya wanawake iliweka msingi wake wa kufuzu mnamo mwaka 2023, walipoichabanga Misri 21-20 katika kombe la FIBA Africa 3×3, na kupata ubingwa wa kwanza kwa taifa katika kiwango cha bara.

Ubingwa huo ulifuatiwa na ushindi mara mbili mfululizo wa nishani ya shaba mwaka wa 2024 na 2025, na kujitangaza kama miamba wa mchezo wa vikapu barani Afrika.

Katika kipindi hicho, timu ya wanaume pia ilionyesha kuimarika, ikitinga awamu ya nusu fainali katika kipute cha 2023 Africa Cup kabla ya kupanda na kumaliza katika nafasi ya 3 bora.

Matokeo hayo yaliimarisha msimamo wa Kenya kwa kuiongezea pointi, kwa wakati mmoja yakiipandisha hadi nafasi ya 2 barani.

Mfumo wa 3×3 umekuwa ukikua kwa kasi tangu kuanzishwa kwenye michezo ya Commonwealth mwaka wa 2022, na kufikia timu 12 kwa kila jinsia.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KENYA YAVUNJA REKODI BARANI AFRIKA MPIRA WA VIKAPU

LIONESSES WAREJEA NCHINI

KENYA YAVUNJA REKODI BARANI AFRIKA MPIRA WA VIKAPU

LOOKMAN AANZA KWA KISHINDO ATLETICO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *