BUNGE LA SIAYA LAPITISHA MSWADA WA KUWALINDA WAJANE
Juhudi za kuimarisha haki za wajane katika kaunti ya Siaya zimepigwa jeki baada ya bunge la kaunti hiyo kupitisha kwa kauli moja mswada wa kuwalinda wajane dhidi ya kudhulumiwa ikiwemo kurithiwa kwa lazima na jamaa za mumewe.
Usajili wa wajane umeratibiwa kuanza baada ya gavana James Orengo kutia Saini mswada huo kuwa sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































