OBURU ADAI ‘AJENDA 10’ ZIMETEKELEZWA
Kinara wa chama cha ODM Oburu Oginga amepuzilia mbali dhana kwamba ajenda 10 zilizoafikiwa baina ya chama hicho na UDA ikiwemo kuwapa fidia waathiriwa wa ukatili wa polisi hazijatekelezwa.
Kwa mujibu Oginga, ripoti kuhusu ajenda hizo inaashiria matokeo ya mkataba huo katika sekta ya ugatuzi, anayosema imetengewa fedha zaidi, huku akidai kwamba tayari bunge limetenga shilingi bilioni 2 kuwafidia waathiriwa.
Ameongeza kuwa fursa za ajira za umma zimeanza kuonyesha ujumuishi wa makabila yote.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































