UPINZANI WADAI KUIBIWA CHAGUZI NDOGO
Viongozi wa upinzani nchini wameendelea kutofautiana na matokeo ya chaguzi ndogo zilizoandaliwa mwishoni mwa wiki jana, wakisema wagombeaji wao ndio walioshinda ila IEBC ikawatangaza wanaoegemea mrengo wa serikali.
Wakiongozwa na Kalonzo Musyoka wa Wiper na Martha Karua wa PLP, viongozi hao wameshikilia kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na haki, na kuwataka wakenya kuwa macho ili hilo lisirudiwe kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































