NYOTA WA STARLETS WAELEZA MATUMAINI YA KUNG’AA WAFCON
Maandalizi ya kikosi cha taifa cha wanawake Harambee Starlets kwa dimba la taifa bingwa barani Afrika kwa wanawake WAFCON 2026 yamepamba moto, huku kikosi cha awali kilichotajwa kikiimarisha mazoezi yake.
Beki wa kikosi hicho Diana Shakava, ameelezea matumaini ya nyota yake nay a kikosi kizima kung’aa katika mashindano hayo yatakayoanza katikakati mwa mwezi ujao nchini Morocco.
Shakava, ambaye alipata nafasi katika kikosi cha awali, ametaja mazoezi ya sasa yanayoendelea kambini kama mazingira mwafaka ya kujifunza ambako wachezaji na makocha wanabadilishana mawazo ya kujenga ushirikiano dhabiti wa timu.
Kulingana nahodha huyo wa klabu ya Ulinzi Starlets, ukufunzi wa kiango cha juu na utangamano na wachezaji wenye tajriba tayari umekuza ustawi wake.
Kikosi cha mwisho kitateuliwa kutoka kwa wchezaji hao mwishoni mwa kambi ya mazoezi kabla ya kusafiri kuelekea Morocco, Kenya ikirejea kwenye dimba hilo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 10.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































