MUSEVENI AONGOZA MATOKEO YA AWALI UGANDA
Rais mkongwe wa Uganda, Yoweri Museveni, ameongoza kwa mbali katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais, huku kukiwa na taarifa kinzani kuhusu visa vya vurugu vilivyoripotiwa baada ya kura kupigwa.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi, Museveni ana asilimia 76.25 ya kura kulingana na kura zilizohesabiwa kutoka karibu nusu ya vituo vya kupigia kura.
Mpinzani wake mkuu, mwanamuziki maarufu Bobi Wine, amepata asilimia 19.85, huku kura zilizobaki zikigawanywa miongoni mwa wagombea wengine sita.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































