HOWE AITAKA NEWCASTLE KUCHEZA MECHI YA MAISHA YAO
Kocha wa Newcastle United, Eddie Howe, ameitaka timu yake kutoa kiwango cha juu kabisa wakati watakaporushiana na FC Barcelona Jumanne katika mechi aliyoiita kuwa kubwa zaidi katika historia ya klabu.
Newcastle watakuwa wakicheza hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League kwa mara ya pili tu, wakikabiliana na vinara wa La Liga katika mkondo wa kwanza wa mchuano huo.
Hata hivyo, baada ya kuiondoa timu ya Azerbaijan, Qarabag FK, katika hatua ya mchujo, Howe amesema kikosi chake kitalazimika kuongeza kiwango ili kuweza kushangaza Barcelona yenye wachezaji nyota chini ya kocha Hansi Flick.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































