SIMBA ATOLEWA MENO KUCHA BUNGOMA
Umaarufu wa kisiasa wa spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula katika kaunti ya Bungoma umewekwa kwenye darubini, baada ya mgombeaji wa kiti cha uwakilishi wadi katika wadi ya Chwele-Kabuchai kupitia chama chake cha Ford Kenya kupoteza kwa mgombeaji huru Eric Wekesa.
Wekesa aliyekuwa akiungwa mkono na gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, amepata jumla ya kura 6,162, huku Vincent Maunda wa Ford Kenya akipata kura 2,765, nao wagombeaji wengine 7 wakipata chini ya kura 100.
Spika Wetang’ula ni mkazi na mpiga kura katika wadi hiyo, wachanganuzi wa kisiasa wakihoji kuwa huo ni mwanzo wa kupoteza umaarufu wake wa kisiasa kwenye kaunti hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































