#Business

MAKAZI YA BEI NAFUU: KENYA YATAMBULIWA KIMATAIFA

Kenya imetambuliwa rasmi kimataifa kwa miradi yake ya makazi ya kijamii kwa watu wasiojiweza na wale wa kadri wa mijini na Mpango wa Kukuza Upya wa Mito ya Nairobi, ambayo imesifiwa kama mipango yenye athari kubwa ya kustahimili hali ya hewa kusini mwa dunia.

Akizungumza katika Kongamano la COP 30 mjini Belem, Brazili, Naibu Rais Kithure Kindiki amesema mashirika ya Umoja wa Mataifa yanapongeza miradi hiyo kwa kutumia rasilimali zinazozalishwa nchini kukabiliana na hatari ya hali ya hewa katika maeneo ya mijini huku ikiboresha hali ya maisha.

Kindiki pia alikaribisha Mpango wa Kujenga Ustahimilivu wa Hali ya Hewa na Mpango wa Watu wasiojiweza Mijini, unaoongozwa na Kenya na Brazili, akisema unalenga kulinda jamii za mijini zilizo hatarini kutokana na mafuriko, ukame na majanga mengine ya hali ya hewa. 

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

MAKAZI YA BEI NAFUU: KENYA YATAMBULIWA KIMATAIFA

RUTO ATETEA AMRI YA “RISASI MIGUUNI’

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *