#Sports

CAF YAMTUZA RUTO


Shirikisho la soka barani Afrika CAF limemtuza Rais William Ruto na tuzo ya kipekee ya ufanisi ya Rais ya mwaka 2025, katika kutambua juhudi zake za kukuza soka nchini na barani Afrika.

Tuzo hiyo ilitolewa nchini Morocco usiku wa kuamkia leo wakati wa hafla ya tuzo za CAF za mwaka 2025, na kupokelewa na balozi wa Kenya nchini Morocco Jessica Gakinya.

Akizungumzia tuzo hiyo, rais wa shirikisho la soka nchini Hussein Mohammed ameelezea matumaini ya kuimarika kwa spoti hasa soka nchini, kutokana na miundomsingi inayowekwa na Rais Ruto.

Marais Yoweri Museveni wa Uganda na Samia Suluhu Hassan wa Tanzania pia walitambuliwa kutokana na mchango wao wa kuimarisha taasisi za soka na kuunga mkono mipango ya mashindano ya bara.

Rais wa CAF Patrice Motsepe, aliwapongeza watatu hao kwa kujitolea kwao katika kuimarisha kandanda barani Afrika.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CAF YAMTUZA RUTO

MSAADA WA AMBULENSI KUTOKA WHO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *