WETANG’ULA ATETEA SHERIA YA KOMPYUTA
Viongozi wanaoegemea mrengo wa Kenya Kwanza wametetea sheria mpya kuhusu matumizi mabaya ya kompyuta na uhalifu wa kimtandao ya mwaka 2025, wakisema sheria hiyo inalenga kulinda walichotaja kuwa ustawi wa jamii.
Viongozi hao walikuwa wakizungumza katika eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wakiongozwa na spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, na kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichung’wa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































