SERIKALI YASISITIZA UMEME UPO
Serikali imewaondolea wakenya hofu ya uhaba wa nguvu za umeme ambao kwa mujibu wa Rais William Ruto, umesababisha kuzimwa kwa umeme katika baadhi ya maeneo majira ya jioni ili kukidhi mahitaji mengi ya bidhaa hiyo.
Kulingana na katibu mkuu katika wizara ya kawi Alex Wacira, taifa lina nguvu za umeme za kutosha, na kauli ya rais ililenga tu kuhimiza uzalishaji zaidi wa nguvu hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































