#Football #Sports

ALIYEKUWA KOCHA HARAMBEE STARS ENGIN FIRAT AFARIKI DUNIA

Kocha wa zamani wa Harambee Stars, Engin Fırat, amefariki dunia kwa kifo cha ghafla kutokana na Mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 56.

Fırat, aliyekuwa akiinoa makali klabu ya Nejmeh SC nchini Lebanon, aliripotiwa kuanguka katika uwanja wa ndege wa Istanbul, Turkey, alipowasili kutoka Beirut.

Mashabiki wa soka nchini Kenya wanamkumbuka Fırat kwa kipindi chake na Harambee Stars kati ya 2021 na 2024, wakati timu ya taifa ilikabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo kusimamishwa kutoka mashindano ya kimataifa na matatizo ya uongozi wa soka nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

ALIYEKUWA KOCHA HARAMBEE STARS ENGIN FIRAT AFARIKI DUNIA

SOKO LA UHURU LABOMOLEWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *