#Local News

UPINZANI WADAI NJAMA YA UBADHIRIFU KUPITIA UBINAFSISHWAJI

Muungano wa upinzani nchini umeibua hofu kuhusu uwepo wa njama ya watu mashuhuri serikalini kunufaika na mpango wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma, na kumtaka Rais William Ruto kuweka wazi mpango huo.

Wakiongozwa na vinara Kalonzo Musyoka wa Wiper, Rigathi Gachagua wa DCP na Eugene Wamalwa wa DAP-K, viongozi hao wamedai kuwa Rais Ruto amekuwa akihusika kibinafsi kwenye mauzo ya baadhi ya mashirika hayo.

Hata hivyo, hawajathibitisha madai hayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *