WAMUTHENDE: NITAWATUMIKIA WOTE
Mbunge mteule wa eneo bunge la Mbeere North Leo Wamuthende, ameahidi kuwaunganisha wakazi wote wa eneo hilo na kutekeleza miradi ya maendeleo bila kujali miegemeo ya kisiasa atakapoanza kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang’anyiro kilicholenga kupima ubabe wa kisiasa kati ya naibu rais Kithure Kindiki na mtangulizi wake Rigathi Gachagua, Wamuthende amewataka wakazi kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kurejea kazini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































