#Football #Sports

ARSENAL WATINGA FAINALI TANGU 2018

Klabu ya Arsenal ya Uingereza imekariubia kushinda taji kuu la kwanza tangu mwaka 2020, baada ya kuitandika Chelsea jumla ya mabao 4-0 na kutinga fainali ya taji la Carabao Cup.

Wakiwa wanaongoza 3-2 kutoka kwenye mkondo wa kwanza wa nusu fainali, the Gunners walisubiri hadi dakika ya 97 kabla ya kujihakikishia tiketi ya kuingia ugani Wembley, nguvu mpya Kai Havertz akifunga bao la pekee katika mechi ya marudiano jana usiku ugani Emirates.

Vijana hao wa Mikel Arteta, ambao wanaongoza ligi kuu ya EPL na wamo katika raundi ya 16 za mwisho ya klabu bingwa bara Ulaya, watamenyana na mshindi kati ya Manchester City na Newcastle ambao watamenyana leo usiku.

Mara ya mwisho kwa Arsenal kucheza fainali ya Carabao ulikuwa mwaka wa 2018, na taji lao kushinda ilikuwa ni FA mwaka 2020.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

ARSENAL WATINGA FAINALI TANGU 2018

KIPKOSGEI BINGWA WA DUNIA RASMI

ARSENAL WATINGA FAINALI TANGU 2018

KANUNI MPYA ZA KRA ZA KUKUSANYA USHURU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *