DUALE AKANUSHA UFISADI KATIKA MAMLAKA YA SHA
Waziri wa Afya Aden Duale amepuuza madai kwamba shilingi bilioni 11 za fedha za umma zimefujwa katika Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) akisema kuwa fedha hizo ni madai yaliyowasilishwa kwa njia isiyofaa na hospitali mbalimbali.
Duale amesema kuwa malipo hayo hayataidhinishwa iwapo stakabadhi zitabainika kuwa za kughushi au zisizokidhi vigezo vilivyowekwa.
Aidha, Waziri huyo ametangaza kuwa SHA italipa hadi shilingi laki tano kwa wagonjwa watakaopata matibabu katika hospitali za nje ya nchi, mradi tu hospitali hizo ziwe na mkataba wa kudumu na mamlaka hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































